Duka la Mangi freshi

Saturday January 7 2017

UKIBAHATIKA kuwa mchezaji kuibuka mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mara tatu, ukirudi Dar es Salaam unafungua duka lako freshi na maisha ya Januari yanasonga kiulaini kabisa.

Wachezaji bora wa mechi na timu hupewa zawadi ya vinywaji vya Azam Malt, jambo ambalo limeonekana kama kejeli kwa washindi.

Kamati ya Kombe la Mapinduzi imekuwa ikitoa zawadi ya katoni tano za kinywaji hicho kwa mchezaji bora wa mechi, katoni nne kwa kila timu na katoni mbili kwa waandishi wa habari huku jopo la makocha wanaochagua mchezaji bora wakipewa katoni moja.

Zawadi hiyo imeonekana kuwa ya aina yake na kuzua mijadala katika makundi ya Whatsapp ambapo watu wengi wamekuwa wakihoji juu ya taswira inayoonekana kutokana na zawadi hiyo.