Dida kumbe bonge la kipa

Muktasari:

  • Kipa ni nahodha wa pili uwanjani lazima awe na tabia ya kujiamini na kutambua kwamba yeye ni kiongozi wa mabeki na hizo sifa Dida anazo

KIPA wa Mtibwa Sugar, Benedictor Tinoco, ameweka wazi kuwa kipa wa Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ ndiye mwenye vitu adimu kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Bara (VPL).

“Hakuna binadamu asiyejifunza kwa mwingine, nimemchunguza Dida, nimebaini utulivu na kujua kupanga mabeki ndicho kinachomfanya awe kipa makini kwenye ligi ya VPL,” alisema kipa huyo ambaye aliwahi kuwa Yanga lakini hakupata namba.

“Kipa ni nahodha wa pili uwanjani lazima awe na tabia ya kujiamini na kutambua kwamba yeye ni kiongozi wa mabeki na hizo sifa Dida anazo na ndicho kinachonifanya nijifunze mengi kwake hana mazoea na kazi yake,” alisema. 

Mbali na hilo alielezea tabia za makipa kwamba ni watu wasiokata tamaa na kudai kuwa ndicho kilichomkuta akiwa Yanga ambako aliishia kusugua benchi lakini kwa sasa akiwa Mtibwa Sugar, anadaka.

“Kipa ni nafasi moja makini tofauti na mchezaji wa ndani ambaye anatakiwa awe na vitu vingi na mifumo yao inabadilika hivyo wanatakiwa wawe na bidii ya kujua vitu vingi zaidi,” alisema.