Dele awagombanisha Xavi, Pochettino

Muktasari:

Pochettino amedai Xavi anajaribu kuwavuruga mastaa wake wakati huu wakiwa katika mbio za kuwania ubingwa wa England na kwamba watawauza wachezaji wao pale tu watakavyoamua kufanya hivyo.

 Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino amedai kwamba kiungo wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez kwa sasa ni adui yake baada ya kukerwa na kauli ya staa huyo wa zamani wa Hispania aliyedai kwamba kiungo wake, Dele Alli anaweza kwenda Manchester City.
Pochettino amedai Xavi anajaribu kuwavuruga mastaa wake wakati huu wakiwa katika mbio za kuwania ubingwa wa England na kwamba watawauza wachezaji wao pale tu watakavyoamua kufanya hivyo.