Chambua: Mechi ya akili sana

Muktasari:

“Yanga ina faida kubwa wakiamua kutumia uzoefu, lakini nao Simba sio wa kuwabeza kwani, hawawezi kukubali kirahisi kufungwa na Yanga tena na isitoshe hawajaonja ubingwa kwa muda mrefu,” alisema.

SEKILOJO Chambua ni mchezaji mstaafu mwenye heshima ya kipekee Tanzania. Amecheza Yanga pamoja na Taifa Stars kwa takribani miaka 10. Amezungumzia mechi ya Simba na Yanga kuwa ni mchezo wa akili sana.

“Yanga ina faida kubwa wakiamua kutumia uzoefu, lakini nao Simba sio wa kuwabeza kwani, hawawezi kukubali kirahisi kufungwa na Yanga tena na isitoshe hawajaonja ubingwa kwa muda mrefu,” alisema.

Chambua alisisitiza kuwa makocha wa timu zote mbili watakuwa na kazi ya kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kutumia nidhamu ya hali ya juu ili kuamua matokeo.

“Kila kocha atakuwa na kazi ya kuhakikisha wachezaji wanatumia vema dakika 90 na pia kucheza kwa utulivu utakaowafanya watumie vizuri nafasi watakazokuwa wanapata za kufika langoni. Hapa ni akili tu,” alisema