Celta Vigo wazima ndoto ya Samatta, Rashford aibeba Man United

Friday April 21 2017

 

By Brussels, Ubelgiji.

Brussels, Ubelgiji. Ndoto ya mshambuliaji wa Tanzania anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta imezimika baada ya timu yake kuaga katika michuano ya Europa League.

Timu hiyo imeaga baada ya kutoka sare ya 1-1 na Celta Vigo katika mchezo uliokuwa wa ushindani wa marudiano uliofanyika kwenye mji wa Brussels, Ubelgiji.

Mchezo wa kwanza timu hizo, Vigo walishinda mabao 3-2 na kwamba kama Genk wangeshinda bao 1-0, wangesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, lakini matokeo ya sare ya 1-1 yanaitupa nje timu hiyo kwa jumla ya mabao 3-2.

Celta Vigo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 63 lililofungwa na Pione Sisto, kabla ya Genk kusawazisha dakika nne baadaye kwa bao la Leandro Trossard.  

Michezo mingine, Rashford Marcus alifunga bao dakika ya 107 lililoipeleka nusu fainali dhidi ya Anderlecht.

Mchezo huo uliingia dakika za nyongeza baada ya kumalizika kwa sare ya 2-2.

Mchezo wa kwanza uliisha kwa sare ya 1-1 lakini jana Henrikh Mkhitaryan alifungia United bao la kuongoza dakika ya 10 kabla ya Sofiane Hanni kuisawazisha Anderlecht kwa shuti la karibu na kufanya matokeo kumalizika kwa sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 za kawaida.  

Manchester United sasa inasubiri kupangiwa ratiba na timu za Celta Vigo iliyoitoa KRC Genk kwa jumla ya mabao 4-3.

Timu nyingine iliyoingia nusu fainali ni Lyon iliyoitoa Besiktas kwa mikwaju 7-6 baada ya sare ya 3-3 huku Schalke ikiitoa Ajax kwa mabao 3-2.