Cavaliers yapambana kufika fainali NBA

Muktasari:

Lengo hilo lilikuwa kushinda baada ya Jumapili kupoteza mchezo wa tatu na kurejesha matumaini ya kucheza fainali ya tatu ya NBA.

Timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers ilianza mchezo wa nne wa fainali ya Ukanda wa Mashariki  ya Ligi ya Kikapu ya Marekani (NBA) dhidi ya Boston Celtics ikiwa na lengo moja la kufika fainali.

Lengo hilo lilikuwa kushinda baada ya Jumapili kupoteza mchezo wa tatu na kurejesha matumaini ya kucheza fainali ya tatu ya NBA.

Kwenye nusu ya kwanza, Cavaliers au Cavs ilitawala mchezo huo. Kuanza vibaya kwa LeBron James  na udhaifu wa safu ya ulinzi uliiwezesha Celtics kuongoza kwa pointi 10 hadi mapumziko, jambo lililowafanya Cavs kujiona  wamemaliza kazi na kupumua.

Kitendo hicho kiliwashtua mashabiki na wapenzi wao na kuwaacha wapinzani wao wakitamba. Pia, hofu ilikuwa uwezo wao wa kupambana na mabingwa wa Ukanda wa Magharibi, Golden State Warriors.

Kipindi cha pili, Cavs walibadili gia, wakiongozwa na Kyrie Irving aliyekuwa na mchezo mzuri na kurudi mchezoni kwa LeBron, Cavs  ilipiga asilimia 71.1 (27 kati ya 38)  na kutawala mchezo, ambao hatimaye ilishinda kwa 112-99. Kwenye mchezo huo, Irving na James waliwafunika Celtics kwa pointi 48-42.

Ushindi huo umewarejesha kwenye mbio za ubingwa wa nne wa Ukanda wa Mashariki na uwezekano wa kucheza fainali ya saba ya NBA kwa LeBron James  na James Jones.

Kwa sasa, Cleveland inaongoza kwa 3-1 na inaweza  kutumia siku sita za mapumziko kabla ya kuanza raundi ijayo Alhamisi kwenye mchezo wa tano utakaofanyika TD Garden