Casillas: Bado nipo nipo kwanza

Saturday December 20 2014

By OLIPA ASSA

KIPA wa Simba, Hussein Shariff ‘Casillas’, amesema licha ya hali yake kuanza kuimarika kutokana na kupona maumivu ya ugoko, lakini hayupo tayari kurejea uwanjani kwa sasa.

Mlindamlango huyo amesema anahitaji kupumzika kwa muda mrefu ingawa amemtaja straika mpya wa Yanga, Amissi Tambwe.

Casillas aliumia ugoko katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini walipoweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa Oktoba 18, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti hivi karibuni, alisema: “Najua Tambwe lazima atakuwa amepania kuonyesha uwezo wake, hivyo makipa wa Simba tutapata usumbufu sana kutoka kwa Tambwe, jamaa anaifahamu kazi yake.”

Kwa mujibu wa Daktari wake, Yasin Gembe, Casillas anatarajia kujiunga na wenzake Januari mwakani kwa sasa kuna mazoezi maalum ambayo wamemwelekeza kufanya nyumbani kwake.