Buffon na Casillas uso kwa uso

Porto, Ureno. Itakuwa mechi inayowakutanisha makipa bora Gianluigi Buffon wa Juventus dhidi ya Iker Casillas wa Porto leo saa 4:45 Usiku.

Pamoja na makipa hao wawili kuelekea mwishoni mwa maisha yao ya soka, Buffon na Casillas kila moja leo wana kitu cha kuthibisha kwamba miaka yao 17 ya soka hayakuwa ya kubatisha.

Buffon mwenye miaka 39, ametwaa kila kitu isipokuwa taji la Ligi ya Mabingwa ambayo mara mbili amemaliza akiwa mshindi wa pili kati mwaka 2003 na 2015, akiwa Juventus.

Wakati Casillas (35) ametwaa mataji yote yakiwamo matatu matatu ya Ligi ya Mabingwa, lakini anapambana kurejea katika kikosi cha Hispania na kuithibisha klabu yake ya zamani ya Real Madrid kuwa walifanya kosa kumtimua miaka miwili iliyopita.

"Kila mchezaji anajua kuwa inachukua muda kuzoa maisha ya mji mpya, watu wapya na maisha mapya," Casillas aliimbia UEFA.com. "Ni kawaida unapokuwa umekaa sehemu moja kwa muda mrefu, ndivyo ilivyokuwa kwangu, itachukua muda kuzoea hapa. Labda kusikifikia kiwango changu kile mwaka jana.

Matokeo yoyote ya mchezo wa kwanza bado Casillas na Buffon wataendelea kuheshimina.

Wawili hao walitumiana ujumbe katika akaunti zao za Twitter hivi karibuni, huku Casillas akimuuliza Buffon, "Unafikiri nani na bora? Kwangu wewe ni bora!!"

Naye Buffon alimjibu, "Sijachangua. Wote ni bora," na kuongezea alama ya sura ya furaha.

Kufanana kwa Casillas na Buffon hakujaishia uwanjani pekee. Makipa hao wawili wachumba zao ni wanahabari.

Casillas anakumbukwa na jinsi alivyombusu Sara Carbonero wakati wa mahojihano baada ya kutwaa Kombe la Dunia  2010 na wawili hao wamefunga ndoa mwaka jana.

Buffon amezaa mtoto na mtangazaji wa Sky Sports, Ilaria D'Amico ambaye bado anajimbulisha kwa jina Buffon.

Pia wachezaji hao wamecheza idadi sawa ya mechi za timu za taifa ikiwa ni michezo167.