Barcelona yamsubiri kocha ValvedeMadrid, Hispania

Muktasari:

Juzi, Bilbao ilishiriki Ligi Kuu Hispania, La Liga ilitangaza kuondoka kwa Valverde, ambaye amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kutua Barcelona ili kuchukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza kuiacha mwisho wa msimu uliomalizika Jumapili iliyopita.

Barcelona yamsubiri kocha ValvedeMadrid, Hispania

Klabu ya soka ya Athletic Bilbao imethibitisha kuondokewa na kocha wake, Ernesto Valverde huku uvumi ukizidi kuenea kuwa atahamia Barcelona.

Juzi, Bilbao ilishiriki Ligi Kuu Hispania, La Liga ilitangaza kuondoka kwa Valverde, ambaye amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kutua Barcelona ili kuchukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza kuiacha mwisho wa msimu uliomalizika Jumapili iliyopita.

 Msimu huo, Bilbao ilimaliza kwenye nafasi ya saba ya Ligi Kuu, La Liga  na inaweza kushiriki Ligi ya Europa msimu ujao lakini ikisubiri mbeleko ya Barcelona kwenye fainali ya Kombe la Mfalme.

Endapo bosi huyo wa Athletic Bilbao atatua Nou Camp anakabiliwa na mtihani wa kuirejeshea taji la ligi ambalo imepokonywa na Real Madrid.

Klabu hiyo ya Nou Camp imetangaza Jumatatu kuwa siku ambayo itamtangaza kocha wake mpya ambaye ataiongoza kufanya pia usajili.

Valverde, 53, ambaye ni mchezaji wa zamani  wa Barcelona anapewa nafasi kubwa kutua kwenye klabu hiyo ya Catalunia