Barca yaingia anga za Real

Muktasari:

Klabu hizo mbili za Barcelona na Real Madrid kwa muda mrefu zimekuwa kwenye mpambano wa chini chini wa kumsajili mchezaji huyo raia wa Brazil.

Klabu ya Barcelona imeongeza dau kwa mchezaji kinda, Vinicius Junior huku mchezaji huyo wa Flamengo akisisitiza mapenzi yake ni kuichezea Real Madrid.

Klabu hizo mbili za Barcelona na Real Madrid kwa muda mrefu zimekuwa kwenye mpambano wa chini chini wa kumsajili mchezaji huyo raia wa Brazil.

Hata hivyo, Real Madrid walifanikiwa kuidaka saini ya mchezaji huyo kwa usajili wa Pauni 45 milioni, huku akiendelea kuichezea klabu yake hadi atakapofikisha umri wa kucheza klabu ya wakubwa.

Vinicius anatarajiwa kutua kikosi cha Real Madrid Julai mwaka 2018.

Pia, klabu ya Flamingo imemuongezea mkataba mchezaji huyo na anatarajiwa kuendelea kuwapo kikosini hadi mwaka 2019.

Vita ya kumuwania mchezaji huyo haijamalizwa na usajili uliofanyika hivi karibuni, badala yake Barcelona wamerudi Flamingo na kuamua kumuongeza dau mchezaji huyo nyota.

Wakala wa mchezeaji huyo, Frederico Pena alisisitiza kwamba mchezaji huyo anahesabika kuwa mchezaji wa miamba wa Hispania, Real Madrid.

Barcelona wamekuja na mbinu mpya baada ya kumtangazia dau jipya ambalo linazidi lile la awali alilosaini na Real Madrid.

ôMtu anaweza akadhani Real Madrid ni vichaa kulipa fedha ya usajili mapema, lakini klabu nyingine imejitokeza kuja kumsajili kwa kuongeza kiwango jambo hilo halikubaliki,ö alisema Pena.