Barca yaichapa Real Madrid kwao

Messi

Muktasari:

Mabao ya Lionel Messi, aliyefunga mara mbili na moja ya Ivan Rakitic yalitosha kwa vijana hao wa Luis Enrique kuibuka na ushindi muhimu

MADRID, HISPANIA
BARCELONA waichapa Real Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu mabao 3-2 na hivyo kupanda hadi kileleni katika msimamo wa La Liga, wakiwa pointi 75 sawa na wapinzani wao hao, lakini wakiwa na wastani mzuri wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Lionel Messi, aliyefunga mara mbili na moja ya Ivan Rakitic yalitosha kwa vijana hao wa Luis Enrique kuibuka na ushindi muhimu iliyokuwa ikiuhitaji kufikia pointi za Real Madrid licha ya kwamba wababe hao wa Bernabeu wapo nyuma kwa mechi moja pungufu. Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Casemiro na James Rodriguez.