Barca, Dortmund zatupwa nje Mabingwa Ulaya

Wednesday April 19 2017

 

By BARCELONA, HISPANIA

BARCELONA na Borussia Dortmund zimetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kupenya kwenye mechi za robo fainali ilizocheza dhidi ya Juventus na AS Monaco. Barcelona iliyocheza na Juventus ilitupwa nje kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya sare ya 0-0 kwenye mechi ya jana Jumatano huko Nou Camp, huku Borussia Dortmund wao wakitupwa nje kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya kuchapwa 3-1 usiku huo wa jana. Katika mechi za kwanza za hatua hiyo ya robo fainali, Barca ilichapwa 3-0 Turin, Italia wiki iliyopita wakati Dortmund wao walichapwa 3-2 kwao Ujerumani.