Arsenal yaonywa kuacha ubahili

Muktasari:

David Seaman aliishauri klabu hiyo alipokuwa akizungumza na mtandao wa Omnisport jana Jumatatu.

London, England. Klabu ya Arsenal imeshauriwa kuwekeza fedha zaidi kwa ajili ya kukijenga kikosi chake ili kuimarika zaidi kwenye Ligi Kuu England msimu ujao.

David Seaman aliishauri klabu hiyo alipokuwa akizungumza na mtandao wa Omnisport jana Jumatatu.

Arsenal imemaliza msimu huu kwenye nafasi ya tano huku wakishindwa kufuzu Ligi ya Mabngwa mwakani kwa misimu 19 wakiwa na kocha Arsene Wenger.

“Ni vyema Arsenal wakafikiria kutumia fedha zaidi kununua wachezaji bora. Iwapo hawatazingatia jambo hili huenda wakashuka zaidi msimu ujao, “ alisema Seaman.