Arsenal yamtega Sanchez kwa Pauni 270,000 kwa wiki

Muktasari:

Hata hivyo, mtandao wa Daily Mail umedokeza kwamba dau halisi analotaka mchezaji huyo ni Pauni 300,00 kwa wiki.

Klabu ya Arsenal imeendelea kupambana ili nyota wake, Alexis Sanchez abaki kikosini hapo baada ya kuamua kumpa ofa ya mshahara wa Pauni 270,000 kwa wiki.

Hata hivyo, mtandao wa Daily Mail umedokeza kwamba dau halisi analotaka mchezaji huyo ni Pauni 300,00 kwa wiki.

Taarifa zaidi zinasema makubaliano hayo yatafanyika kwa undani baada ya mechi ya fainali ya Kombe la FA itakayochezwa dhidi ya Chelsea kesho Jumamosi.

Mchezaji huyo inaelezwa licha ya kuwapo taarifa mbalimbali za kuhamia Bayen Munich, lakini anafaurahia zaidi maisha ya soka akiwa jijini London.