Arsenal yagonga mwamba kwa Keita

Friday May 19 2017

Munich, Ujerumani. Kocha wa klabu ya RB Leipzing, Ralph Hasenhuttl amesema  kiungo wake Naby Keita haendi kokote msimu ujao licha ya kuwapo taarifa Arsenal kuhitaji huduma yake.

Timu hiyo ambayo imemaliza nafasi ya pili kwenye Ligi ya Ujerumani ya Bundesliga, imefuzu kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwa maana hiyo mchezaji huyo, ana nafasi ndogo kwenda Arsenal ambayo bado inahaha kufuzu mashindano hayo makubwa barani Ulaya.

Mchezaji huyo raia wa Guinea huenda akazima ndoto za klabu za Liverpool na Arsenal zilizoonyesha nia ya kumhitaji.

“Anajisikia vyema kuendelea kucheza klabu za Ujerumani. Pia tunampenda na ijulikane kwamba kocha ametumia rasilimali nyingi kuwekeza kwake ili mchezaji bora,” alisema kocha Hasenhuttl.