Amber Rose amtetea Kanye West

Amber Rose na Kanye West

Muktasari:

MWANAMITINDO Amber Rose ambaye kwa sasa anatamba na kipindi chake cha televisheni cha The Amber Rose Show, ameibuka na kumtetea mpenzi wake wa zamani, rapa Kanye West ambaye amewahi kuingia katika mzozo na Taylor Swift.

NEW YORK, MAREKANI. MWANAMITINDO Amber Rose ambaye kwa sasa anatamba na kipindi chake cha televisheni cha The Amber Rose Show, ameibuka na kumtetea mpenzi wake wa zamani, rapa Kanye West ambaye amewahi kuingia katika mzozo na Taylor Swift.

“Mimi si shabiki mkubwa wa Kanye,” alianza kwa kusema kabla ya kuendelea: "Hata hivyo nakumbuka nilikuwa karibu naye katika tukio la mwaka 2009 Kanye alipodaiwa kumbughudhi Swift na nalikumbuka tukio zima lilivyokuwa.

"Nakumbuka mama na baba wa Taylor walikuja karibu yetu na kusema, Kanye kuna siku utakuwa na mtoto wa kike na watu watakufanyia hivyo wewe.''

"Kanye alikuwa mnyonge, alijisikia vibaya kwa sababu hakuwa na tatizo lolote na Taylor.''

Kanye na Amber wamewahi kuwa wapenzi miaka ya nyuma kabla ya kuachana, Kanye kwa sasa ni mume wa Kim Kardashian.