Real yatoa macho kwa Alaba

Muktasari:

Inadaiwa kuwa Rais wa Madrid, Florentino Perez aliongea na mabosi wa Bayern Munich wakati wa pambano la baina ya timu hizo katikati ya wiki iliyopita akionyesha kumtaka mlinzi huyo, mwenye asili ya Nigeria lakini mwenywe anaitaka zaidi Barcelona.

LICHA ya Real Madrid kumfukuzia kwa kasi mlinzi wa kushoto wa Bayern Munich, David Alaba inadaiwa kuwa staa huyo wa kimataifa wa Austria anapenda zaidi kujiunga na Barcelona licha ya kwamba, bado haijaonyesha nia ya kumchukua.

Inadaiwa kuwa Rais wa Madrid, Florentino Perez aliongea na mabosi wa Bayern Munich wakati wa pambano la baina ya timu hizo katikati ya wiki iliyopita akionyesha kumtaka mlinzi huyo, mwenye asili ya Nigeria lakini mwenywe anaitaka zaidi Barcelona.

Wakati huohuo, Real Madrid imekataa dau la pauni 42 milioni za Liverpool kwa ajili ya kumchukua winga, Marco Asensio ambaye amekuwa akitesa Santiago Bernabeu na kuziba vema pengo lililoachwa na staa, Gareth Bale ambaye ni majeruhi.

Asensio (21) ni mmoja kati ya makinda wanaokuja juu katika soka la Hispania na katikati ya wiki iliyopita alifunga bao moja katika pambano la robo fainali la LIgi ya mabingwa wa Ulaya.