Kumbe Kaseja kahusika tuzo ya Aishi Manula

Muktasari:

“Kim akiwa kocha Stars, mwaka 2012 alikuwa ananijumuisha katika kikosi chake,   ila alikuwa akiniambia ameniita si kwa ajili ya kucheza bali kujifunza kwa kina Kaseja.’’

KIPA wa Azam, Aishi Manula amesema mafanikio yake yametokana na kupitia kwenye mikono ya makipa bora kama   Juma Kaseja, Ally Mustafa ‘Barthez’ Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mwidini.

“Kaseja, Mwidini, Dida na Barthez ni baadhi ya makipa ambao nimejifunza mengi kwao hasa nilipokuwa nakutana nao Taifa Stars, nadhani kwa sasa watakuwa wanafurahia kuona nimefanyia kazi maelekezo yao,” alisema.

Manula alisema bahati ya kukaa na kina Kaseja ilitokana na juhudi za kocha  Kim Poulsen ambaye alikiona kipaji chake akiwa timu ya taifa ya vijana na akaamua kumchanganya na wakongwe.

“Kim akiwa kocha Stars, mwaka 2012 alikuwa ananijumuisha katika kikosi chake,   ila alikuwa akiniambia ameniita si kwa ajili ya kucheza bali kujifunza kwa kina Kaseja.’’