Kylie Jenner: Mimi wala si mjamzito

Muktasari:

Katika habari hiyo, Kylie mwenye umri wa miaka 18 anadaiwa kuwa na ujauzito na baba anayetajwa kuwa wa mtoto mtarajiwa ni Tyga, ambaye tayari wameachana.


DEMU wa zamani wa rapa, Tyga, Kylie Jenner ameibuka na kukanusha habari kwamba yeye ni mjamzito.

“Umekuwa ni uvumi huu huu kwa miaka mingi sasa na hakuna mtoto yeyote, kwa hiyo nikifikia hatua hiyo nitakuwa wa kwanza kuwaambia,’ alisema.

Katika habari hiyo, Kylie mwenye umri wa miaka 18 anadaiwa kuwa na ujauzito na baba anayetajwa kuwa wa mtoto mtarajiwa ni Tyga, ambaye tayari wameachana.

Mara ya kwanza Kylie kuambiwa mjamzito ilikuwa Desemba 2014 wakati huo akiwa na miaka 17, lakini alitoa jibu la mkato: “Sijaribu kuwa rapa, siolewi na sina ujauzito.’’ Hata hivyo, miezi mitano baadaye uvumi huo uliibuka upya na mrembo huyo kujibu tena. “Watu wamekuwa wakifikiria ni mjamzito kwa miezi minane sasa, jamani ukweli ni kwamba mimi si mjamzito”.

Uvumi mwingine ambao uliibuka kabla ya huu wa ujauzito ni ule uliodai kwamba, Kylie amemaliza matatizo yake na Tyga na kwamba, kwa sasa lao moja na hivyo kuibuka dhana kuwa ujauzito ndio uliowafanya wapatane.

Uvumi wa awali ulikuja baada ya Kylie kuonekana akiwa amevaa pete mpya iliyonakshiwa kwa madini ya almasi, lakini habari za ndani zilidai kuwa Tyga na Kylie hawakuchumbiana.

Habari hizo ziliendelea kudai kwamba Kylie amekuwa akimzungumzia Tyga kwa marafiki zake na pia amewahi kuzungumza na Tyga kuhusu masuala la uchumba na ndoa na kubwa analofikiria ni maisha ya baadaye na Tyga.

Tyga, ambaye amezaa mtoto na mwanamitindo, Blac Chyna, aliachana na Kylie sababu mojawapo ikiwa kitendo cha  kaka yake Kylie, Rob kutoka na Chyna na kwa sasa wana mpango wa kufunga ndoa na wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.