Mariah Carey hataki ustaa kwa wanawe

Muktasari:

Kwa sasa Mariah na mapacha wake wako mapumzikoni, Cannes, Ufaransa pamoja na mchumba wake James Parker, ambaye huenda wakafunga naye ndoa. Tangu kuzama kwa bilionea huyo, Mariah amekuwa utulivu kwelikweli.

MWANAMUZIKI, Mariah Carey amesema anapenda watoto wake waishi maisha ya kawaida badala ya yale ya ustaa.

Mwanamuziki huyo mwenye watoto mapacha wenye umri wa miaka mitano, Moroccan na Monroe aliozaa na mume wake wa zamani, Nick Cannon alisema: “Nataka wajione wa kawaida, wasiwe watu wa kumulikwa kila kona, hawatatakiwa kusafiri duniani kote japo wanapenda kusafiri kwa ndege, nikiwaacha nyumbani siku tano tu wanauliza lini tutapanda ndege.