ABC yausaka ubingwa kikapu

Muktasari:

  • Msimu mpya wa RBA umeanza huku Savio wakiwa ni mabingwa watetezi kwa wanaume

Kocha wa ABC, Duruweshi Shamuni  ameendelea kutamba na kikosi chake  kwa kuifunga UDSM  Insider kwa pointi 94-65 katika mchezo wa Ligi ya mpira wa kikapu kanda ya Dar es Salaam (RBA).

ABC imeonekana  kuwa moto wa kuotea mbali kwenye msimu huu mpya  wa 23 kwa  wanaume huku kwa wanawake ukiwa ni wa 21 kwa kupata matokeo ya ushindi katika michezo yao miwili mfululizo.

Kwenye mchezo wao wa kwanza ABC walianza kwa kuifunga Kurasini Heat kwa pointi 71- 42.

“Tulijua namna ya kucheza nao ndiyo maana hawakutupa shida, kuanzia kwenye eneo letu mpaka kwenye eneo lao, uharaka ulitusaidia kwenye kutengeneza mashambulizi yetu,” alisema Duruweshi.

Mchezo mwingine ulichezwa Ijumaa usiku ulishudia Oilers ikichapa Tanzania Prisons kwa pointi 91-57.