Man City yajitosa kwa Griezmann

Muktasari:

  • Mfaransa huyo amekuwa katika orodha ya wachezaji wanaowaniwa na mahasimu wao Manchester United, lakini Pep Guardiola sasa ameonyesha nia ya kumtaka nyota huyo.
  • Taarifa hiyo inachochea moto kuwa Sergio Aguero hayupo katika mipango ya Guardiola pamoja na Kun kuwa na rekodi nzuri ya ungaji ndani ya Etihad.

London, England .Manchester City imeingia katika mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann.

Mfaransa huyo amekuwa katika orodha ya wachezaji wanaowaniwa na mahasimu wao Manchester United, lakini Pep Guardiola sasa ameonyesha nia ya kumtaka nyota huyo.

Taarifa hiyo inachochea moto kuwa Sergio Aguero hayupo katika mipango ya Guardiola pamoja na Kun kuwa na rekodi nzuri ya ungaji ndani ya Etihad.

Gazeti la The Daily Mail limeripoti kuwa Guardiola amehamisha akili zake kwa nyota wa Atletico baada ya kushindwa kufikia malengo yake ya kumbadilisha Aguero  kushindwa kufua dafu.