Sky Sports yamsimamisha Carragher

Muktasari:

Beki huyo wa zamani wa Liverpool alifanya kosa kwa kumtemea mate binti akiwa kwenye gari

London, England. Mchambuzi wa Sky Sports, Jamie Carragher amesimamishwa baada ya kitendo chake cha kumtemea mate msichana mwenye  umri wa miaka 14.

Carragher aliyelipwa pauni1milioni kwa mwaka alifanya kitendo hicho wakati binti huyo akiwa na baba yake wakati alipokuwa akiendesha Range Rover baada ya kushudia Liverpool ikichapwa 2-1 na Manchester United Jumamosi iliyopita.

Alionekana katika taarifa ya habari Sky News muda mfupi baada ya kusimamishwa, Carragher alitazama video aliyorekodiwa akifanya kitendo hicho wakati wa mahojiano ya juu ya tukio hilo.

Ilikuwa kidogo adondoke chini wakati alipokuwa akihojiwa na Sarah Hewson katika TV, alijitahidi kujieleza ili kunusuru kibarua chake na heshima yake kubwa aliyotegeneza.

Alisema kitendo hicho alisema alifanya kama “mtu aliyechanganyikiwa", aliongeza: "Sina cha kujitetea nimefanya jambo lililotia fedhehe familia yangu na watu wangu wote wa karibu."