Okwi:Kila mechi kwetu fainali

Muktasari:

Okwi anasema anaona ligi ina ushindani wa juu, ambapo kila timu ina malengo yake, jambo linalowafanya waheshimu kila mchezo ili kupata pointi tatu.

STAA wa Simba, Emmanuel Okwi amesema kila mechi kwao ni fainali, akianimini kwa kufanya hivyo kutawasaidia kufikia malengo ya ubingwa.
Okwi anasema anaona ligi ina ushindani wa juu, ambapo kila timu ina malengo yake, jambo linalowafanya waheshimu kila mchezo ili kupata pointi tatu.
Amezungumzia mchezo wao na Mwadui kwamba hautakuwa rahisi hivyo wanahitaji nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kushinda mechi hiyo.
"Si mchezo mwepesi lakini tutajituma kadri tuwezavyo ili tuweze kufikia malengo yetu ya kupata pointi tatu ugenini,"anasema.