Singida United kufuata nyayo za Simba, Yanga

Muktasari:

Tangu Singia United itue 16 Bora ya Kombe baada ya kuifunga Green Warriors kwa penalti 4-3 hivi karibuni, imekuwa na mipango ya kuiwezesha kufika mbali zaidi kimataifa.

Dar es Salaam. Timu ya Singida United inayonolewa na kocha Hans van Der Pluijm imekuwa na mipango ya kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho (FA).

Tangu Singia United itue 16 Bora ya Kombe baada ya kuifunga Green Warriors kwa penalti 4-3 hivi karibuni, imekuwa na mipango ya kuiwezesha kufika mbali zaidi kimataifa.

Awali, Kocha Pluijm alisema anaiwamani na kikosi chake ambacho kimekuwa kwenye nafasi nzuri kwenyemsimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 30.
Ni wazi kwamba iwango Singida United ikifanikiwa kufikisha malengo yake ya kutwaa ubingwa wa FA inaweza kufika kwenye nyasi za kimatifa huku wachezaji wakipata fursa ya kupanda ndege.

Simba na Yanga ndio wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa inayotarajiwa kuchezwa mwezi huu.