Mechi ya Yanga Kombe la Shirikisho yapangwa

Muktasari:

Hata hivyo robo fainali ya Kombe la Shirikisho inatarajia kuanza kutimua vumbi Ijumaa ya Machi 30 ambapo utachezwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Stand United dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa CCM Kambarage.

Dar es Salaam. Timu ya Yanga itatupa karata yake kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho siku ya Jumapili, Aprili 1 kwenye Uwanja wa Namfua watakapokwaana na Singida United.

Hata hivyo robo fainali ya Kombe la Shirikisho inatarajia kuanza kutimua vumbi Ijumaa ya Machi 30 ambapo utachezwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Stand United dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa CCM Kambarage.

Machi 31 2018 Tanzania Prisons itakutana na JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine Mbeya. Pia Azam FC itakuwa inacheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Yanga imesafiri kwenda Botswana alfajiri ya leo Jumanne tayari kwa machezo wa marudiano wa Ligi ya Mabigwa Afrika, huku ikiwa imeondoka kifua mbele baada ya kuondoka nchini kuifua mbele kwa kuifikia Simba pointi 46 kileleni.