Makomandoo Singida United, Mbao FC wawashiana moto

Muktasari:

Mbao ndio walianza kuwasili uwanjani majira saa 8:30 mchana ikiwa imelindwa na makomandoo wao,huku Singida wakiongozwa na gari la Kocha Mkuu, Hans Pluijm wakatinga saa 8:45 mchana.

Kabla ya mechi kuanza kati ya Mbao FC na Singida United, vurugu baina ya makomandoo wa timu hizo wamezua vurugu wakati magari ya wachezaji yakiwasili.
Mbao ndio walianza kuwasili uwanjani majira saa 8:30 mchana ikiwa imelindwa na makomandoo wao,huku Singida wakiongozwa na gari la Kocha Mkuu, Hans Pluijm wakatinga saa 8:45 mchana.
Vurugu zilianza pale Singida walipokuwa wakiwasili,ambapo mashabiki wote 'Makomandoo' wa timu hizo walijipanga getini zinapoingilia timu uwanjani na kuanza kuzozana huku ngumi zikitembezwa.
Hata gari la Singida United lilipofika eneo la mlango wa chumba cha kubadilishia nguo wachezaji, ilishuhudiwa ngumi na mikong'oto ikitembezwa kwa wawili hao,huku mawe yakirushwa hovyo.