VIDEO: Simba noma! Yazima jaribio la kumuondoa Jonesia

MECHI YA SIMBA NA AZAM YAMUIBUA MWENYEKITI WA WAAMUZI (FRAT)

Muktasari:

Habari ambazo zilipatikana juzi Jumatatu zilisema kuwa mwamuzi Emmanuel Mwandembwa ndiye angechukuwa nafasi ya Jonesia lakini baada ya taarifa hizo kuvuja imeelezwa kwamba Simba hawakukubaliana na mabadiliko hayo ya ghafla.

Dar es Salaam. Wakati jana ikiwepo na taarifa za chinichini za mabadiliko ya waamuzi wa mechi ya  leo Jumatatno kati ya Simba na Azam FC sasa mwamuzi wa mechi hiyo atabaki kuwa Jonesia Rukyaa kama ratiba ilivyokuwa imepangwa awali.

Habari ambazo zilipatikana juzi Jumatatu zilisema kuwa mwamuzi Emmanuel Mwandembwa ndiye angechukuwa nafasi ya Jonesia lakini baada ya taarifa hizo kuvuja imeelezwa kwamba Simba hawakukubaliana na mabadiliko hayo ya ghafla.

Hivyo mechi ya kesho itachezeshwa na Jonesia akisaidiana na washika vibendera waliokuwa wamepangwa pamoja Sudi Lila na Helen Mduma wote wa Dar es Salaam. Wakati kwenye mabadiliko washika vibendera walikuwa ni Lila na Mohammed Mkono