Okwi ajimilikisha mabao Uwanja wa Taifa

Muktasari:

Bao hilo la kwanza  lilifungwa dakika 36 kwa shuti  Mganda huyo akiunganisha krosi iliyopigwa na Said Ndemla na kuiwezesha Simba kufikisha pointi 41.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ameifungia timu yake bao lililoipaa ushindi na kuifanya kujiimarisha zaidi kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Bao hilo la kwanza  lilifungwa dakika 36 kwa shuti  Mganda huyo akiunganisha krosi iliyopigwa na Said Ndemla na kuiwezesha Simba kufikisha pointi 41.
Simba ambayo ilifanya mashambulizi ya mara kwa mara kupitia zaidi kwa Okwi dakika 28  shuti lake lilitoka nchi chache kutoka kwenye mwamba wa goli.
Simba walifanya mashambulizi mengine dakika 23 kwa Okwi shuti lake likadakwa na dakika ya 24 Shomari Kapombe akapaisha.
Dakika ya 13 beki  wa Simba Yusuph Mlipili anafanya kazi ya ziada kuokoa shambulio la hatari la Azam akatoa nje.
Simba walifanya mashambulizi Yao wqkitokea zaidi pembeni kwa Shiza Kichuya, Said Ndemla na Okwi.
Pia kwa azam wakimtumia Mbaraka Yosuph Enock aliisumbua mara kadhaa safu ya ulinzi ya Simba lakini bahati haikuwa upande wao.