Simba kazi moja kwa Al Masry Machi 9

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, watashuka kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa kuikabili Township Rollers Machi 6 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mabadiliko ya ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pia Simba itaivaa Al Masry kwenye Uwanja wa Taifa Machi 9 lakini awali ratiba ilikuwa ikionyesha mchezo huo kupigwa Machi 6.

Msimu huu CAF imebadili kalenda yake ambapo michezo yote ya Kimataifa ngazi ya vilabu itapigwa katikati ya wiki huku ile ya ligi ya mabingwa ikipangwa siku za Jumanne na Jumatano kama ilivyo Ulaya.