Karia azipa somo Simba, Yanga mechi za kimataifa

Muktasari:

Huku akiitaka Yanga ijitahidi kufanya marekebisho kwa mapungufu yaliyoonekana walipocheza na St Louis, licha ya kushinda bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallece Karia amezishauri klabu za Simba na Yanga, kutojibweteka kwa ushindi walioupata nyumbani, akiwataka wajiandae vya kutosha kwa mechi za ugenini ili waweze kufika mbali zaidi.

Huku akiitaka Yanga ijitahidi kufanya marekebisho kwa mapungufu yaliyoonekana walipocheza na St Louis, licha ya kushinda bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

"Simba wasijibweteke kwa ushindi wa mabao 4-0, wakaona wamemaliza kila kitu, kwani wana safari ndefu, hivyo wajipange kikamilifu kwa ushindi mnono mpaka ugenini,"

"Yanga bado wana nafasi nzuri, wajipange naamini kikosi kina wachezaji wenye uwezo na michuano ya kimataifa kwani wameshiriki mara nyingi, naamini wakizingatia hayo watafika mbali,"anasema.

Karia anasema anaamini mwaka huu, klabu za Simba na Yanga zinaweza kufika mbali kinachotakiwa ni kuongoza umakini na kuwasoma wapinzani wao ili waweze kuwa fiti na mechi hizo.
"Tusiishi kwa kukariri kuona hatuwezi kufika mbali kwenye michuano hiyo,naamini tukijituma kwa bidii, tuna nafasi ya kusonga mbele na kuandika historia nyingine kwa washindani wetu,"anasema.