Sare yampa jeuri kocha Simba

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amesema uwezo walioonyesha wachezaji wake jana anaamini wana nafasi ya kushinda mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry itakayochezwa Misri.

Simba ilitoka sare ya mabao 2-2 na Al Masry jambo linalomfanya Mfaransa huyo kuamuamini inawezekana kwenda kushinda Misri, akisisitiza wanahitaji kuenda kimbinu zaidi.

"Ni kweli kipindi cha kwanza timu ilitaka kuteleza kidogo, lakini tulipozungumza nao baada ya mapumziko walirejea uwanjani kwa kasi na wachezaji walijituma wakionyesha nia ya kuhitaji matokeo,"

"Naamini tungeweza kushinda na kufanya vema isingekuwa kukatika kwa umeme na mvua kuanza kunyesha, lakini hayo yamepita hayawezi kujirudia, tunaangalia tufanye nini mbele ya safari,”alisema Mfaransa huyo.