Sanchez ni suala muda tu Man United

Mshambuliaji nyota wa Arsenal Alexis Sanchez

London, England. Klabu ya Manchester United inatarajia kukamilisha usajili wa mshambuliaji nyota wa Arsenal Alexis Sanchez muda mfupi ujao.

Sanchez anatarajiwa kutua Old Trafford kwa Pauni180 milioni na atajifunga mkataba wa miaka minne na nusu kwa mashetani wekundu.

Man United imepiga kumbo majirani zao Manchester City iliyokuwa ikimtaka muda mrefu, lakini iliishia njiani baada ya Arsenal kudai dau kubwa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, anatarajiwa kubadilisha na nahodha wa Armenia Henrikh Mkhitaryan kama sehemu ya makubaliano.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho, amemtaja Sanchez kuwa ni mchezaji mpiganaji anayeweza kuamua matokeo uwanjani.