Real yamtolea macho Pogba

Muktasari:

  • Kiungo huyo Mfaransa ameshindwa kuonyesha ubora wake katika mechi za hivi karibuni.

London, England. Real Madrid ipo tayari kumsajili Paul Pogba, lakini wanatakiwa kutoa zaidi ya pauni120milioni kwa Manchester United.

Real ilimkosa kiungo huyo wakati alipoamua kwenda Manchester United kwa uhamisho ulivunja rekodi ya dunia ya pauni 89milioni mwaka 2016.

Lakini rais wa Bernabeu kwa sasa wapo tayari kurudi upya na kumchukua Pogba mwisho wa msimu huu.

Real imepoteza makali yake katika La Liga msimu huu, lakini imekuwa kifuatilia mwenendo wa kiungo huyo ndani ya Man United baada hivi karibuni kutolewa nje na Jose Mourinho baada ya kuonyesha kiwango cha chini.

Kiungo huyo mwenye miaka 24, ndiyo kwanza yupo katika mwaka wake wa pili katika mkataba wake wa miaka mitano ndani ya Man United, ambao hawana mpango wa kuuza.

Kama kutakuwa na mabadiliko ndani ya Old Trafford, basi miamba hiyo ya Hispania watalazimika kutoa zaidi ya pauni 120m.

Kubwa litategemea na hali ya mchezaji mwenyewe, kama ataondoa hali ya kutojisikia vizuri katika msimu huu.

Mfaransa huyo alitolewa wakati Man United ikipojea kipigo kutoka kwa Tottenham mwezi uliopita pia aliachwa benchi dhidi ya Huddersfield.

Pia, Pogba alibadilisha wakati wa mchezo dhidi ya Newcastle.

Wakiwa nje, Mourinho amekuwa akimuunga mkono nyota huyo na kumsifia kwa jinsi anavyojitoa kwa timu.