Real, Kane, Messi kikaangoni Ulaya

Monday February 12 2018

 

Madrid, Hispania.Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano itaanza leo na kesho kukiwa na maswali nane yaliyotawala midomoni mwa watu yanayotaka majibu sahihi.

 1. Jinsi gani Real Madrid watamzuia Neymar?

Edinson Cavani, Kylian Mbappe na Neymar wametegeneza safu hatari ya ushambuliaji Ulaya; Watatu hao kwa pamoja wamefunga mabao 25 katika mechi za Ligi ya Mabingwa msimu huu wakiwa na wastani wa mabao 4.17 kwa mechi.

Hilo ni jambo linalotisha zaidi kwa sasa ambako mabingwa watetezi wanatatizo kubwa katika safu yao ya ulinzi huku wakiruhusu kufungwa nyumbani.

2. Harry Kane ataivunja ngome ya Juventus?

Harry Kane yuko katika kiwango cha juu kwa sasa Ulaya, kasi yake ya ufungaji imekuwa ni gumzo hasa wakati huu anapokwenda Turin. Hapo kabla Tottenham Hotspur ilikuwa haijafika hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa, lakini kikwazo kikubwa kwao ni ukuta imara wa miamba hiyo ya Italia.

Juventus ‘The Old Lady’ wameruhusu bao moja tangu Novemba 19, 2017; Je? Kane atafanikiwa kuivunja ngome hiyo.

3. Liverpool wataendelea kufunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa?

Liverpool haipewi nafasi ya kusogelea ubingwa mwaka, hata hivyo Jurgen Klopp amebadilisha hali hiyo kutokana na vijana wake kufunga mabao mengi. Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wote wapo katika kiwango cha juu na walifanya yako katika mchezo dhidi ya Southampton wakishinda 2-0 jana.

Tatizo kubwa  la Liverpook ni safu yake ya ulinzi jambo linalopa wakati mzuri Porto katika mchezo huo.

4. Pep Guardiola ataendeleza rekodi yake ya kucheza nusu fainali?

Manchester City ilitolewa kwa mara ya kwanza katika hatua ya mtoano na Monaco msimu wa 2016/17 ikiwa ni mara ya kwanza kwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona kuondoa katika hatua hiyo katika Ligi ya Mabingwa.

Vinara hao wa Ligi Kuu England watakuwa na kibarua kizito mbele ya FC Basel katika mechi hizo mbili muhimu.

 5. Messi atavunja mwiko kwa Chelsea hoodoo?

Chelsea dhidi ya Barcelona ni moja ya mechi za kuvutia zaidi za Ligi ya Mabingwa, hata hivyo Lionel Messi hajawahi kufunga bao dhidi ya klabu hiyo ya London katika mechi saba zilizopita.

Barcelona imesonga mbele mara sita kati ya mechi hizo saba, lakini Chelsea wanajivunia rekodi ya kumzuia nyota huyo wa Argentina. Katika mechi nane alizocheza dhidi ya Chelsea, Messi amepiga mashuti 29, hajafunga bao lolote.

6. Sevilla itavuka raundi ya 16 dhidi ya Manchester United?

Sevilla wamefanikiwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora mara nne katika misimu ya karibuni, lakini walifanikiwa kusonga mbele mara ya mwisho 1958. Tayari walishatolewa na Fenerbahce mwaka 2008, CSKA Moscow (2010) na Leicester City (2017).

Kocha  Jose Mourinho na Manchester United anawasubili kwa hamu Wahispania hao katika mchezo huo.

 

7. Bayern Munich ipo katika kiwango cha juu, wanaweza kutwaa ubingwa?

 Tangu aliporejea  Jupp Heynckes kikosi cha Bayern kimekuwa moto wa kuotea mbali. Wamepoteza mechi tatu tu katika mashindano yote kwenye Uwanja wa Allianz Arena na kuwafanya kuwa timu pekee inayoshiriki Bunderliga tangu 2016 ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani.

8. Roma watamaliza matatizo yao ya kushindwa kutanda katika hatua kubwa?

Roma imefuzu kwa hatua ya mtoano wakiwa vinara juu ya Chelsea na Atletico Madrid, hayo ni mafanikio makubwa kwa miamba hiyo ya Italia.

Roma imeshinda mechi tatu kati ya 10 zilizopita za hatua hiyo na sasa watawaku na kibarua dhidi ya Shakhtar Donetsk.