Infantino ataka kupiga ‘stop’ usajili wa mkopo

Muktasari:

  • Rais wa Fifa wiki ijayo atakuwa Tanzania kwa ajili ya mkutano wa kupanga ajenda za mkutano mkuu wa Fifa.

Rais wa Fifa, Gianni Infantino anataka kufanya mapinduzi makubwa katika mfumo wa usajili wachezaji duniani ili kuleta usawa na uwazi zaidi.

Rais Infantino amepanga kuunganisha pamoja mambo 11, katika kuhakikisha mfumo wa usajili unakuwa bora zaidi.

Infantino anataka kuona dirisha moja la usajili litakalofanyika  Juni na kufungwa kabla ya ligi kuanza.

Pia anataka kuzui klabu kuwatoa wachezaji kwa mkopi bila ya kuwa na ukomo kama walivyofanya Udinese ambayo wachezaji wake 103, wanacheza sehemu nyingine kwa mkopo.

Rais huyo wa Fifa pia anaamini suala la mishahara ya wachezaji linapaswa kuwa katika mstari ambao unaendana na mapato ya klabu ili kufanya ligi zenye ushindani bora zaidi.

"Hali ilivyo kwa sasa ni nzuri kuna fedha nyingi, lakini jinsi mambo yanavyokwenda yatia shaka mbeleni," alisema Infantino.

"Tunatakiwa kuchukua hatua, tunatakiwa kulinda misingi iliyofanya soka kuwa hapa lilipo."

Mwisho, Infantino pia anataka kuwepo kwa sheria nzuri itakayowasimia mapato wanayopewa mawakala na wasimamizi wa uhamisho kwa sababu kwa mwaka jana pekee kiasi cha euro 400milioni kati ya euro 5.1 bilioni ikilikwenda kwa mawakala.