Pluijm akubali mziki wa Simba

Muktasari:

Pluijm alisema kufanya makosa mengi mbele ya timu kubwa kama Simba ndio kilichochangia kufungwa magoli mengi, lakini wamejifunza kitu.

KOCHA wa Singida United, Hans Van Pluijm, amekiri kikosi chake kilikuwa na mapungufu hasa katika safu ya ulinzi ndiyo maana walikumbwa na kipigo cha aibu cha mabao 4-0 mbele ya Simba juzi Alhamisi.

Pluijm alisema kufanya makosa mengi mbele ya timu kubwa kama Simba ndio kilichochangia kufungwa magoli mengi, lakini wamejifunza kitu.

“Simba walikuwa bora zaidi yetu katika mechi hii na kama watakuwa wanacheza kama hivi katika mechi zinazokuja, watafanya vizuri zaidi ya hapa,” alisema Pluijm.

“Simba ina wachezaji makini na wazoefu na hili linaweza kuwa shida au faida kwao pale wanapokutana na wachezaji ambao hawana uzoefu wa ligi,” alisema Pluijm ambaye tangu ameanza kufundisha soka nchini hajawahi kufungwa mabao zaidi ya mawili.