Owen: Sanchez umepotea kwenda Man U

Muktasari:

Mourinho hana rekodi nzuri ya wachezaji waopenda kushambulia katika kikosi chake

London, England. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Michael Owen anaamini  Alexis Sanchez amefanya uamuzi mbaya wa kujiunga na miamba hiyo ya jiji la Manchester.

Mshambuliaji huyo wa Arsenal yuko katika hatua za mwisho za kuhamia Old Trafford.

Mshambuliaji huyo wa Chile ameondoka Arsenal akibadilisha na kiungo Henrikh Mkhitaryan aliyeondoka Man United.

Sanchez (29), amekuwa akitoa mambo ya uhamisho wake katika mtandao wa Instagram akitupia picha zake akiwa kwenda ndege akielekea Kaskazini Magharibi.

Hata hivyo, Owen amedai Jose Mourinho si kocha wa kupata kitu kikubwa zaidi kutoka kwa Mchile huyo.

"Sijavutiwa na Jose jinsi anavyoweza kuwatumia wachezaji wanaopenda kushambulia zaidi katika kipindi hiki kigumu kwake.

"Nafikiri kama ukiangalia upande wa pili wa Pep Guardiola, baadhi ya wachezaji wake wamebadilika sana, mfano ni Sterlings unaona jinsi alivyokuwa bora chini ya Mhispania huyo.

"Ukiangalia washambuliaji wote wenye vipaji waliopita kwa Jose Mourinho katika miaka yote, sidhani kama wamefanikiwa na kuwa washambuliaji bora wa kidunia.

Owen alimtumia Anthony Martial kama mfano wa wachezaji bora walioshindwa kuthibisha ubora wao chini ya kocha huyo Mreno.