Nsajigwa atuliza mizuka ya mashabiki Yanga

Muktasari:

  • Yanga ni mabingwa mara 26 wa Ligi Kuu Tanzania ikiwa ndiyo timu yenye mafanikio zaidi tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo 1965

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema timu ipo kwenye kipindi cha mpito, ila anaamini yataisha na watatetea ubingwa wa msimu huu.

Akifafanua kauli yake Nsajigwa anasema bado wana mechi 16 mbele yao, hivyo wana nafasi ya kuendelea kujipanga kuhakikisha wanachukua ubingwa kwa mara nne mfululizo.

"Kutoka sare na Mwadui FC na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu, haimanishi tumefika mwisho wa kupambania ubingwa, bado safari ni ndefu, wachezaji ambao wanaumwa watakuwa wamerejea katika afya zao,"alisema.

Nsajigwa amewaomba mashabiki wa timu hiyo, kutokubali kukata tamaa badala yake aliwataka wawe bega kwa bega na timu, ili kuweza kuyafikia malengo yao.

"Unapokata tamaa unamfanya mpinzani wako awe na nafasi, kikubwa mashabiki waendelee kuunga mkono timu pamoja na kuwapa moyo wachezaji,naamini tutafika tu," alisema Nsajigwa.