Nsajigwa: Tatizo la washambuliaji wetu hawajiamini

Muktasari:

Yanga ipo nafasi ya tatu kwa sasa na pointi 25 ambazo ni sawa na Mtibwa iliyo ya nne,  Azam FC ndiyo vinara wana pointi 30, wakifuatiwa na Simba iliyo ya pili na pointi 29.

Dar es Salaam. KOCHA msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema, kikosi chao kinapoteza nafasi nyingi za mabao   kwa sababu washambuliaji wao hawajiamini wanapofika eneo la hatari.

Nsajigwa amesema, wachezaji wanacheza vizuri kwa ushirikiano na wanafika eneo la hatari la wapinzani wao, kinachowashinda huwa ni kufunga mabao tu.

"Tatizo linalowasumbua wachezaji wetu ni kutojiamini kila wanapokuwa eneo la kufunga mabao, wanacheza wanatengeneza nafasi lakini kosa kosa ndiyo zimekuwa nying. Kama wangekuwa wanajiamini na kuamini wanachokifanya, tungefunga mabao mengi tu,"anasema Nsajigwa.

"Hata hivyo, tatizo hili lilikuwepo hapo nyuma tukalifanyia kazi na sasa limejirudia tena, tunakwenda kulifanyia marekebisho na mechi ijayo naamini mambo yatakuwa mazuri."

Kwa sasa Yanga ipo nafasi ya tatu na pointi 25,  ambazo ni sawa na Mtibwa iliyo ya nne, Simba ni

ya pili ina 29, wakati Azam FC ndiyo vinara wana 30.