Mwadui, Ndanda zatoka sare

Muktasari:

Kutokana na matokeo hayo Mwadui imefikisha pointi 14 na kusalia nafasi ya tisa  kwenye msimamo wa ligi.

Mwadui imelazimisha sare ya bao 1-1 na Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga.

Ndanda ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa John Tiba kabla ya Mwadui kusawazisha kupitia kwa Awadh Juma.

 Kutokana na matokeo hayo Mwadui imefikisha pointi 14 na kusalia nafasi ya tisa  kwenye msimamo wa ligi wakati Ndanda imepanda hadi nafasi ya 10 kwa kufikisha pointi 13.