Msanii wa Bongo Muvi Johari afiwa na mama yake

Muktasari:

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na rafiki ya Johari wa karibu, Mike Sango ambaye amesema taarifa zaidi zitatolewa baada ya ndugu zake kukusanyika.

Dar es Salaam. Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi leo Jumatano mchana na msiba utakuwepo Mburahati Barafu jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya awali inaeleza kuwa msiba wa mama huyo wa msanii utakuwa maeneo ya Mburahati na ndugu jamaa na marafiki wanaendelea kumfariji kwenye mitandao ya kijamii.

 Mungu ailaze roho ya  marehemu mahala pema peponi, amina. Endelea kuwa nasi hapa kwa habari zaidi.