Mnigeria wa Njombe asaka timu kimtindo

Muktasari:

Njombe Mji kwa sasa ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara

Dar es Salaam. Beki wa Njombe Mji, Mnigeria Ahmed Tajudeen amesema anataka kuhakikisha anafanya vizuri akiwa na klabu hiyo kabla ya kusaka timu nyingine.

Tajudeen aliliambia Mwanaspoti online, anataka kuhakikisha Njombe Mji ifanye vizuri katika michezo iliyobaki ndio ajiangalie upande wake.

"Huwezi ukasema unaondoka sasa hivi kama timu ikifanya vibaya naangalia mbele sana, lakini ni lazima timu ifanye vizuri katika michezo iliyobaki," alisema Mnigeria huyo.

Tajudeen alisema amesaini Njombe, baada ya kupata nafasi katika klabu hiyo, lakini anaamini kwamba safari yake ya soka bado inaendelea.

"Naamini kabisa kwamba safari yangu ya soka bado inaendelea ndani na nje ya Tanzania, nilisaini Njombe kwa sababu hapa ndio nilipata nafasi ya kusajili baada ya kufanya majaribio na kufuzu," alisema beki huyo.