Mikono ya Shirko yawabeba Diamond Platnumz, Yamoto Band

 Maisha popote ili mradi mkono uende kinywani ndivyo  alivyofanya produzya Shirko.

Shirko jina lake halisi ni Awadh Salim Awadh ni mwenyeji wa Mombasa kwa sasa anafanya shughuri zake jijini Dar es Salaam.  

Ni mmoja wa watayarishajiwa ngoma kali zilizoweza kuwafanya vijana wa Kitanzania kuvuma ndani na nje ya bongo Diamond Platnumz, Yamoto Band pamoja na Asley.

Asilimia kubwa ya kazi alizotia mikono yake ziliweza kukubalika na zipo zinazoendelea kukubalika na kuwaweka wasanii husika kwenye chati kama Dogo Asley na ngoma yake ya ‘Natamba’ ambayo imeweza kufanya vizuri na kumuwezesha kuchukua tuzo ya jiwe la mwezi mara mbili mfululizo kuliko msanii yeyote wa Tanzania.

Shirko ametayarisha ngoma nyingi ambazo zimeweza kufanya vizuri ndani ya bongo na nje pasipokuweka mashabiki kumtambua kutokana na kutokuweka sign yake.

“Wengi walilalamika sana kwa nini nilikuwa siweki alama yangu katika nyimbo nilizotengeneza, wengine wakashindwa kujua kama nimetengeneza mimi,”anasema Shirko

Nyimbo alizotengeneza na kutamba ni pamoja na ‘kidogo’ aliyoimba Diamond Platnumz kwa kushirikiana na P Square, ‘my sweetysweety’ ya Chege Chigunda akishirikiana na Run town, ‘Sugua gaga’ ya Shaa, pamoja na nyimbo za Yamoto Band zote kasoro ya ‘Cheza kwa madoido’ alizitengeneza yeye na hazikuwa na alama yake kama zilivyo za watayarishaji wengine kwa sababu alikuwa chini ya kampuni zilizomilikiwa na watu wengine kama Mkubwa na Wanawe.

Baadhi ya vitu watu wasivyovifahamu

Mwanaspoti: Kwanini uliamua kufanya kazi Tanzania na siyo nyumbani (Kenya)

Shirko: Nilijitahidi kufanya kazi Kenya, lakini walichelewa kukubali kipaji na uwezo wangu matokeo yake Tanzania wakanipokea vyema na mwisho na mwisho wa siku Kenya walipoona nimeanza kusikika wakawa wanashindwa kujua mimi ni wa wapi wakidhania ya kuwa mimi ni Mtanzania.

Mwanaspoti: Kati ya muziki wa Kenya na Tanzania unapenda upi,

Shirko: Napenda wa Tanzania kwa sababu kuna ushindani hawana hiyana kujali huyu ni maarufu au mchanga, wanapokea kila mwenye uwezo na ndio maana kila leo tunaona vipaji vipya na tangu miaka ya nyuma ila Kenya walichelewa sana kutambua uwezo wa wasanii wachanga ndio sababu tasnia ikadidimia.

Mwanaspoti: Wewe umekaa Kenya unaona wengi wanapenda mziki gani kule?

Shirko: Kutokana ana wao kutotambua muziki wa wasanii wachanga wasanii wengi waliona fursa kwenye muziki wa gospel na wengi wakakimbilia huko na kujipatia umaarufu hadi kufikia hatua ya kufanikiwa.

Mwanaspoti: Wewe unapenda mziki wa Tanzania au Kenya?

Shirko: Nitakuja kuupenda mziki wa Kenya kipindi watu wakiacha kudharaliana, kuoneana gere, tamaa kwa upande wa wadau na kusapoti muziki wa wasanii wachanga na kusapotiana kama Kenya na siyo kimkoa fulani na hii inadidimiza sanaa ya Kenya kwa kiasi kikubwa na wajifunze kupitia wanaoendesha muziki wa gospel ndipo nitaupenda ila kwa sasa nimeupa talaka moja.

Mwanaspoti: Akitokea msanii wa Kenya anataka kufanya kazi na wewe utampokea?

Shirko:Nawapenda wasanii wenzangu na mimi ni mwanamuziki na mtayarishaji sina hiyana napenda muziki mzuri na wasanii wazuri wafike mbali.

Mwanaspoti: Ni mbinu gani ambazo ulizitumia ili kuubadili mziki wa Kenya?

Shirko:Nilifungua milango siku nyingi watu waje kufanya kazi na mimi ilka wengi wanataka kunitumia kama chambo cha kuwakutanisha na wasanii fulani ndipo waje wafanye kazi na mimi na sio kuamua kufanya kazi zao wenyewe,isiwe mtu anataka kufanya kazi na Asley ndipo waanze kunitafuta

Mikakati ya 2018

Shirko anasema amemaliza mkataba na Mkubwanawanae na kufungua studio yake ambayo itakuwa jijini Dar es Salaam “Vibe Records Tanzania” na itamuwezesha kufanya anachotaka na kupenda kwa uhuru wa kutengeneza muziki autakao.

Shirko anasema Asley ni mwanamuziki wa kwanza kurekodi katika studio hiyo na bado anazo nyimbo nyingine anaendelea kurekodi ila ambaye anategemewa kuja kwa kwa surprise na kasi kubwa ni hali ya juu ni mkongwe Berry Black mashakiki wake mkao wa kula,

“Mashabiki hawatasikia tena kufanana kwa muziki sababu nitakuwa natengeneza inavyotakiwa na siyo kumridhisha kiongozi. Nitaikuza brand yangu na jina la studio na maproducer wengine kupitia kila nyimbo na mafanikio pia yataanza kuonekana sasa sababu ya kuwa na mpango kazi,”anasema Shirko

Nyimbo alizowahi kuimba Shirko mwenyewe akiwa kama collabo au group artist ni ‘Nawewe tu’ pamoja na ‘Najua’akiwa na 2Berry, ‘Kumbe ni mwizi’akiwa na AT, Gelly wa Rhymes, ‘Happy birthday’ akiwa na Yamoto band, ‘Asikutoe roho’ akiwa na AmouryBaby na ‘Kicheche’ akiwa na Amoury Baby na Asley.