Meya wa Kinondoni amkubali kocha Minziro

BAADA ya klabu ya Kmc kufanikiwa kupanda ligi kuu, maneno mengi yakianza chini kwa chini kwamba kocha mkuu Fred Minziro anaweza akaondolewa katika timu hiyo kama ambavyo ilikuwa huko nyuma katika vilabu alivyopitia.

Akifafanua tetesi hizo Mstahiki Meya wa KMC, Benjamini Sitta alisema wao wanaendelea nae kwa msimu ujao huku wakimuongezea nguvu kulingana na matakwa yake.

"Tunajua huko nyuma alikuwa akipandisha na kuondolewa hivyo sisi tunasema kwamba bado tupo nae katika ligi kuu," alisema.

Akizungumzia mipango yao katika kuleta nyota wa kigeni, alisema watamsikiliza kocha na idadi yake kisha ndio watamtekelezea.

"Tunajipanga kwasababu tumepanda daraja, tunachokifanya sisi ni kumsikiliza yeye kama atataka tuongeze watu katika benchi, kama anataka wachezaji wa kigeni tutamsikiliza mwalimu," alisema.

Minziro aliipandisha Singida United msimu uliopita, lakini aliondoka klabuni hapo baada ya kushindwa kufikiana makubaliano.