Mechi sita pointi moja yageuka balaa Mbeya sita

Mbeya. Straika wa Mbeya City, Mohamed Mkopi amesema hawawezi kurudia makosa waliyofanya kwa mechi zilizopita ya  kutopata pointi tatu kwa kila mechi kati ya michezo  sita waliyocheza hivi karibuni.

City itakutana na Lipuli FC leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa na Straika huyo amesema kwa ushirikiano na wachezaji wenzake wamejipanga kuchukua pointi tatu.

Mkopi alisema hata wachezaji inawauma kuona kati ya pointi 18 walizostahili kukusanya katika michezo hiyo, wao wanaambulia pointi moja inayowafanya wajione siyo kitu mbele ya mashabiki na wadau wao.

Alisema, “Sijawahi kushuhudia jinamizi la namna hii, lakini siku zote asiyekubali kushindwa huyo siyo mshindani. Tunajipanga kufuta makosa yote keshokutwa tutakapokutana na Lipuli.

Straika huyo aliyewahi kukipiga Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar, alisema wanajua ubora waliokuwa nao Lipuli ingawa ni wageni kwenye ligi hiyo lakini lazima wapigwe.