Dayo alivyozima ndoto ya Mavugo kucheza kimataifa

Tuesday February 13 2018

 

By Albert Kasigara (Msomaji)

Dar es Salaam. Ndoto ya Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Laudit Mavugo kuitumikia klabu ya Simba kwenye mechi za kimataifa (CAF- Confederation Cup) imezimwa na mchezaji Dayo Antonio Domingos.
Unamkumbuka Dayo Antonio Domingos Mshambuliaji wa klabu ya Ferreviario ya Msumbuji alitaka kujiunga na klabu ya Simba kwa dakika za mwisho jina lake likachomolewa baada ya rais wa klabu ya Ferreviario ambaye ni meneja wake kumkataza kujiunga na Simba.
Usajili wa Dayo ndani ya klabu ya Simba, alikuwa anakuja kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo ambaye klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi walipanga kumpeleka kwa mkopo. Baada ya Dayo kushindwa kujiunga na klabu ya Simba klabu hiyo iliamua kubaki na Laudit Mavugo.
Wakati hayo yakifanyika, Simba walikuwa wametuma majina ya wachezaji ambao watacheza mechi za kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho bila jina la Mavugo ambao walipanga kumtema na nafasi yake ingechukuliwa na Dayo.

-Baada ya dili la Dayo kushindikana Simba walijaribu kuongeza majina ya wachezaji wapya huko CAF na mojawapo ya jina liliongezwa ni la Laudit Mavugo ambaye  jina lake halikupitishwa na CAF kutokana na dosari kwenye kutuma jina lake na ndio maana Hata mechi ya Jumamosi dhidi ya Gendarmerie National hukuliona jina lake.

-Ndoto ya Mavugo kuitumika klabu ya Simba kwenye mechi za kimataifa ni kuiombea klabu ya Simba iweze kufika hatua ya Makundi ambapo vilabu vinaruhisiwa kuongeza wachezaji. Kwa sasa kikosi cha Simba kimataifa kitakuwa kinawategemea washambuliaji Emmanuel Okwi, John Bocco, Nicholas Gyan na kinda Moses Kitandu.asubui njema