Mbongo apumzishwa Ujerumani msimu mzima

Wednesday January 10 2018

 

By By THOMAS NG’ITU

MBONGO,  Emily Mgeta anayekipiga klabu ya VFB Eppingen inayoshiriki Ligi Daraja la tano nchini Ujerumani, amepewa mazoezi maalumu ili asiongezeke kilo, licha ya kutakiwa kupumzika msimu mzima.

Mgeta aliumia bega katika mechi na akafanyiwa upasuaji ,  uongozi wa klabu yake umeamua kumpatia mtaalamu wa kumuangalia ili asiongezeke uzito.

“Huku wanajali sana mchezaji kukaa nje kwa msimu mzima kibongo bongo unaweza usipate vitu muhimu katika timu, lakini hapa nimepewa mwalimu wa kunifanyia mazoezi maalumu ili kulinda mwili wangu nisiongezeke kwa sababu nitakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima,” anasema.

Mgeta anaeleza, mazoezi ambayo hivi sasa anayafanya ni kwenda gym na kocha ambapo anapewa mazoezi ya kunyonga baiskeli, kukimbia ndani ya wiki moja dakika thelathini na tano na dakika arobaini na tano mara mbili.

“Naweza kukimbia mfano Jumatatu jioni au mchana pia nikanyonga baiskeli dakika Hamsini, Alhamisi nikakimbia dakika thelathini na tano jioni, ijumaa namalizia arobaini na tano, kasha Jumamosi nikaingia gym kufanya mazoezi mengine.