Mbaya wa Simba awaita Yanga

Tuesday January 9 2018

 

By THOBIAS SEBASTIAN

Zanzibar. Winga wa URA, Kalama Deboss aliyeifunga Simba juzi amesema imefurahishwa kuifunga timu kama hiyo na anajipanga ili kuifunga na Yanga kwenye mechi ijayo. 

Deboss alisema kwanza anacheza ili kunisaidia timu yake kupata ushindi, lakini atahakikisha anacheza vizuri nikipata nafasi ya kufunga kwenye mechi ya Yanga kama ilivyokuwa dhidi ya Simba. 

"Kuzifunga timu kubwa za Simba na Yanga unajijengea heshima kubwa kama mchezaji wa hapa Afrika Mashariki jambo hilo ndio ambalo na mimi natamani kukufanya pia," alisema. 

"Ila hata Kama nikashindwa kupata nafasi ya kufunga nitajaribu hata kuwatengenezea wenazngu ili kufunga kwani wote nia yetu ni moja," alisema Deboss.

Deboss ndio alizamisha matumaini ya Simba kukonga hatua ya nusu fainali baada ya kuwafunga goli moja kwenye mechi yao na Simba kuondolewa nje ya mashindano.