Njombe Mji yafungua makucha Kombe la FA

Muktasari:

Mchezo huo uliokuwa wa hatua ya 16 bora umepigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe na wenyeji kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata.

Dar es Salaam. Mshindi wa pili kombe la FA (ASFC) msimu uliopita, Mbao FC wameondolewa na Njombe Mji kwa changamoto ya penalti 6-5 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliokuwa wa hatua ya 16 bora umepigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe na wenyeji kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata.
Njombe ndio walitangulia kupata bao dakika ya 39 kupitia kwa Ditram Nchimbi na Mbao kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Said Said.
Mbao ambao msimu uliopita walifanikiwa kufika fainali na kisha kuondolewa na Simba kwa mabao 2-1,leo wamejikuta wakifungashiwa virago bila majibu.
Kwa matokeo hayo,Njombe wanatinga hatua ya nane bora ya michuano hiyo,huku Mbao wakiaga rasmi.